Burudani

Lulu Diva atema cheche, akataa mazoea

Msanii wa Bongo fleva Lulu Abas ‘Luludiva’,  ametoa onyo kali kuhusu matumizi mabaya ya jina lake na kauli zisizo na heshima zinazoelekezwa kwake na kusema kwamba sheria itafuata mkondo wake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lulu Diva ameandika kuwa ukimya wake haumaanishi ni ujinga au upumbavu, bali ni njia ya kujiheshimu binafsi na kuwataka wahusika kutengua kauli vinginevyo sheria itafuata mkondo wake.
“Kuna muda nakaa kimya ila haimaanishi mimi ni mjinga au mpumbavu ila naamua kuwa kimya kwa kujilinda na kujiheshimu binafsi ila sasa naona naonekana kama zoba kwa kutaka kutrend kwenu kutumia jina au maneno kuhusu mimi.
 
Nimechoshwa na nimechoka tabia hizo ikiwemo baadhi ya media na Wasanii Kwa kauli mbaya na za kuchafuliwa.
 
Nimesikitishwa na kauli za Msanii Lavalava dhidi yangu zisizo na heshima Dhidi Yangu.
Nahisi sasa ni muda wa kila mmoja kumuheshimu mwenzake na kutokuchukuliana poa.
 
Sheria itachukua mkondo wake kwenye hili, na mkome mara moja. Sio ombi, ni lazima sheria itafuatwa…. Nimechoka” ameandika Lulu Diva.

Related Articles

Back to top button