Ligi Kuu

Mpanzu katili sana aisee!

DAR ES SALAAM: Mpanzu mbona kama hizi sasa sifa! sikia nikuambie licha ya kiwango bora alichoonesha juzi kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar winga wa Klabu ya Simba, Elie Mpanzu amewataka wanasimba kuwa na subira ili aoneshe kipaji chake kwa kucheza kwa mafanikio na kuipatia mafanikio timu yake.

Kwa kauli ya Mpanzu ni sawa na kusema amejitathimini na kuona bado hakuwa kwenye ubora anaotaka yeye hivyo anasema Wanasimba watafurahia huduma yake huko Msimbazi.

Mpanzu alionesha kiwango kizuri katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar na kuisaidia timu yake kupata ushundi wa mabao 5-2 mchezo uliopigwa Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Katika mchezo huo mpanzu alicheza kwa dakika 57 tu lakini mashabiki wa Simba walisifu kiwango chake wakiamini kuwa atakuwa silaha muhimu katika mafanikio yao msimu huu.

Mpanzu amesema bado hajapata mechi nyingi za kucheza anaimani kuwa kila atakapopata nafasi ya kucheza ataonesha kiwango kizuri na kusaidia timu yake.

“Kwa sasa mapema sana kuzungumza bado sijaanza kucheza mechi nyingi za ligi, kikubwa nikuhakikisha nashirikiana na wenzangu kufikia malengo tunayotarajiwa na wanasimba,” amesema.

Mpanzu amekiangalia kikosi cha Simba kimataifa ambapo amesema hana mashaka na timu hiyo kucheza robo fainali ya kombe la Shirikisho Afrika.

Amesema hakuwa kwenye mipango ya michezo iliyopita ya kimataifa lakini anaona jinsi wachezaji wenzake wanavyopambana na kuhimizana wanapokuwa kambini.

“Nilikuwepo uwanjani nikishuhudia wenzangu wakipambana kutafuta alama tatu muhimu katika michezo ya Kimataifa, wanapambana na wamejitoa na kufanikiwa kupata matokeo jambo ambapo linanipa imani kuwa inawezekana kutikisa kwenye michuano hiyo”

Mpanzu anakuwa ingizo jipya la kwanza Simba katika dirisha dogo la usajili licha kutambulishwa miezi miwili iliyopita kipindi dirisha likiwa limefungwa lakini sasa yupo huru kukupiga na uzi wa mnyama.

Related Articles

Back to top button