Nyumbani

Yanga Princess, Fountain heshima Uwanjani

YANGA Princess imesema mchezo wake wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Fountain Gate katika michuano ya Kombe la Samia hautakuwa rahisi kesho wanawaheshimu wapinzani na kujipanga kufanya vizuri.

Yanga itacheza huo wa kwanza dhidi ya timu ya Fountain Gate kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Kocha Mkuu wa Yanga Princess Edna Lema amesema wapinzani wake wako vizuri hivyo, kwa kutambua ubora wao amewaandaa wachezaji kimbinu kupata matokeo mazuri.

“Tumejianda vizuri na tunaamini utakuwa mchezo mzuri na mgumu wa ushindani, tunawaheshimu wapinzani wetu ni wazuri, lakini uzuri ni kwamba nimewaandaa wachezaji wangu kuhakikisha tunafanya vizuri,”amesema.

Edna amesema hakuna majeruhi wapya zaidi ya Ariet Udong anayemalizia matibabu yake ili arudi tena uwanjani. Kukosekana kwake amesema haiwasumbui kwa kuwa ana uhakika na timu yake itapata matokeo.

Nahodha Irene Kisisa amesema “Kwa niaba ya wachezaji tumejianda vizuri naamini katika mchezo wa kesho tutafanya vizuri kutokana na mazoezi na maandalizi tuliyofanya”

Kocha Mkuu wa Fountain Gate Mirambo Camil amesema timu yake imejiandaa vizuri, inakwenda kukutana na Yanga ambao walikutana kwenye ligi na kuona ni kwa namna gani walishindana nao.

Naye nahodha wa Yanga Princess Aquila Gaspa amesema anaamini wanaenda kucheza kwenye maelekezo ya walimu ambayo wamewapatia wakiwa tunajua kabisa ni mchezo wa matokeo ni mchezo ambao wanahitaji kushinda ili kwenda hatua inayofuata.

Related Articles

Back to top button