Ligi Kuu

Mudathir Yahya akabidhiwa Mamelod

UONGOZI wa Yanga SC na benchi la ufundi, umeamua kumkabidhi kiungo wao Mudathir Yahya, mechi ya mkondo wa kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Taarifa hiyo imetolewa leo na ofisa habari wa  timu hiyo Ali Kamwe wakati akizungumza na waandishi wa habari.

“Uongozi na benchi la ufundi wameazimia kwa pamoja kuwa mchezo wetu dhidi ya Mamelodi Sundowns, akabidhiwe kijana kutoka Kizimkazi, Mudathir Yahya,” amesema Kamwe.

Kamwe amesema kauli mbiu yao katika mchezo huo ‘SimuZiiteTutukutaneKwaMkapa’

“Kazi ambayo tunayo kuanzia sasa hivi ni kupiga simu kwa watu wote tuwaambie tukutane kwa Mkapa,” amesema Kamwe

Related Articles

Back to top button