Ligi Kuu

Mashujaa FC wavunja benchi la ufundi 

KIGOMA: UONGOZI wa Mashujaa FC, umevunja  benchi la ufundi la timu hiyo  na kuachwa kwa kocha mkuu Mohammed Abdallah ‘Bares’ inadhihirisha changamoto kubwa inayoikumba klabu hiyo.

Imeelezwa kuwa uamuzi huu unadhihirisha kwamba viongozi wa timu wanajaribu kufanya mabadiliko ili kuboresha matokeo, hasa baada ya kipigo kutoka kwa Singida Black Stars.

“Ingawa uamuzi huu wa kuvunja benchi la ufundi ni wa kawaida katika dunia ya soka, unakuja na shinikizo kubwa kwa viongozi kuleta mabadiliko ya haraka ili kurejesha ufanisi.

Kama ilivyo kwa timu nyingi, changamoto za kutoridhisha matokeo hufanya uongozi kuchukua hatua kali kama hii, sasa huenda Mashujaa FC itahitaji mkakati mpya wa kiufundi na utendaji ili kuleta mabadiliko chanya,” amesema.

Mtoa habari huyo amesema  inaweza kuwa fursa kwa viongozi wa timu na wachezaji kuonesha juhudi mpya na kuongeza ari ya kushinda katika mechi zijazo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button