Mashindano ya gofu ya KCB yatimua vumbi

Shindano la Wazi la “KCB East Africa Golf Tour”limeanza rasmi siku ya Leo katika Klabu ya Gofu ya ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Dar es Salaam.
Akizungumza na Wanahabari hii Leo, Meja Jenerali Ibrahim Mhona, Mkuu wa Utendaji Kivita na Mafunzo amesema, Lugalo Gofu imekuwa ikiwandaa Watoto kwa ajili ya timu ya Gofu kwa miaka ijayo.
“Nawapongeza watoto kwa Mchezo mzuri waliocheza pia ni maandalizi mazuri kwa timu ya watoto kwa miaka ijayo na naipongeza KCB Bank kwa kuunga Mkono Juhudi hizo na kuandaa kupitia shindano la “KCB East Africa Golf Tour”,amesema Meja Jenerali Ibrahim Mhona (Mkuu wa Kivita na Mafunzo JWTZ)
Kwa Upande wake Cosmas Kimario, Mkurugenzi Mkuu wa KCB Tanzania amesema, Leo wamefungua rasmi shindano la ‘KCB East Africa Golf Tour’ na michuano inaendelea ili kupata washindi.
“Shindano la East Africa Golf Tour lilikuwa na lengo la kupata wachezaji wanne watakaoiwakilisha Tanzania kwenye fainali nchini Kenya mwezi Desemba na matarajio yangu ni kuwa Wachezaji hao wataibuka kidedea.” Amesema Kimario
Naye Alli Kayombo Nahodha wa Timu ya Watoto (Juniors) Lugalo Gofu amesema, wanashukuru kwa kupata fursa ya kushiriki Shindano hilo kwani inaongeza Chachu ya kukuza vipaji vyao katika Mchezo wa Gofu.