FeaturedGolf

‘Lugalo Golf Fundraiser’ kusisimua gofu kwa watoto

DAR ES SALAAM: KATIKA kukuza mchezo wa gofu nchini, @lugalo_golftanzania Klabu ya Gofu ya Lugalo imeandaa ‘Golf Fundraiser’ shindano lenye lengo la kuchangia timu ya watoto ‘juniors’ linalotalajiwa kufanyika Mei 11 mwaka huu katika viwanja vya Gofu jijini Dar es Salaam.

Ofisa Habari wa Lugalo Gofu, Meja Selemani Semunyu amesema, miundombinu ya viwanja ipo vizuri licha yakuwepo upepo na mvua za hapa na pale ila wao kama klabu inawakaribisha wachezaji.

“Tunawakaribisha wachezaji na wadau wote kushiriki shindano na kuunga mkono harambee hiyo ya kuchangia timu ya watoto lengo likiwa ni kusaidia kukuza vipaji vya Watoto,”amesema Meja Semunyu

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenza klabuni hapo, Neema Chibanila amesema, wamejipanga kuelekea kwenye shindano na wapo tayari kuwapokea wachezaji kutoka vilabu mbali mbali.

“Tupo tayari kuwapokea wageni kutoka mataifa mbalimbali kwaajiili ya kushuhudia mchuzo huu wa Gofu utakaosaidia kuzalisha na kukuza vipaji vipya,” amesema Chibanila.

Related Articles

Back to top button