Muziki

Marioo: “Sikumdharau mtu, nilisema ukweli”

DAR ES SALAAM: MSANII wa Bongo Fleva, Omary Mwanga ‘Marioo’, ameweka sawa kauli yake iliyozua gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kusema kuwa Bongo Fleva haisikiki kwa kiwango kikubwa nchini Marekani.

Kauli hiyo iliwafanya baadhi ya mashabiki kuhusisha maneno yake na Diamond Platnumz, wakidai kuwa Marioo amemdharau msanii huyo kutokana na mafanikio yake katika muziki wa kimataifa.

Hata hivyo, Marioo amefafanua kuwa hakuwa na nia ya kumdharau wala kumlenga Diamond, bali alikuwa akitoa mtazamo wake kuhusu hali ya Bongo Fleva katika soko la Marekani.

“Mimi nimeamaanisha kile nilichokiongea. Sikuwa na maana tofauti, sikuwa na maana yoyote mbaya, sikuwa na maana ya kumdharau mtu, ila nilikuwa nasema tu ukweli,” amesema Marioo

Kauli hiyo imeendelea kuibua mijadala miongoni mwa mashabiki, huku mjadala mkubwa ukiwa ni kuhusu kiasi ambacho Bongo Fleva imeweza kufika katika soko la muziki la Marekani na nafasi ya wasanii wa Tanzania katika kupeleka muziki huo kimataifa.

Related Articles

Back to top button