Sopu mmoja tena Azam FC

DAR ES SALAAM: MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Abdul Suleiman ‘Sopu’ ameongeza mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuitumikia kikosi cha matajiri hao chamazi.
Taarifa kutoka Azam FC imeeleza kwamba nyota huyo bado yupo sana kwenye viunga vya Azam Complex hadi 2026 baada ya kuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja.
Ikumbukwe Mkataba wa Sopu na Azam FC ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu wa 2025/25 kulingana na ubora wa anaonyesha uongozi wa Azam FC umeonyesha dhamira ya kumbakiza ndani ya viunga vya Chamazi.
Mshambuliaji huyo hajaonekana uwanjani muda mrefu kutokana na majeraha aliyoyapata na amekuwa nje ya Uwanja takribani wiki tatu baada ya kuumia kifundo cha mguu, katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Zimamoto Uwanja wa New Amaan Complex, Visiwani Zanzibar.