Majaliwa kushuhudia Knockout ya Mama

DAR ES SALAAM: WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika pambano la Knockout ya Mama linayotarajia kuchezwa Desema 26, katika ukumbi wa Seper Dome uliopo Masaki, Dar es Salaam.
Siku hiyo kutakuwa na mapambano 13 ya kimataifa na matano watawania mikanda ikiwemo ubingwa wa (WBO Global’, WBC Afrika ,WBF international, na IBA Intercontinental.
Mabondia watakaowania mikanda hiyo ni Yohana Mchanja atapigania mkanda wa WBO dhidi ya Mei Farjado wa Ufilipino, Said Chino atatea ubingwa wa IBA intercontinental.
Ibrahim Mafia atatea mkanda wa WBC Afrika dhidi ya Lusizo Manzana wa Afrika Kusini, Salmini Kasim atawania mkanda wa WBF International dhidi ya Adrian Lerasan na Kalolo Amiri atatea ubingwa wa PST dhidi ya Sihle Jelwana wa India.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni, Saad Mtambule kuwa kutokana na ukubwa wa pambano hilo la kumsapoti Rais Samia Suluhu Hassan wanatarajia Waziri Mkuu Majliwa kuwa mgeni rasmi wa pambano hilo.
“Nafurahi tunaenda kumaliza mwaka kivingine kabisa kwa kishindo siku ya Desemba 26 kuna pambano kubwa litakaowaleta pamoja wadau wa ngumi na utaleta mtazamo mpya katika mchezo huo.
Kutokana na ukubwa wa pambano hilo tunatarajia kupata ugeni kutoka kwa Waziri Mkuu, Majaliwa kuja kushuhudia pambano hilo la Knockout ya Mama,”amesema.
Mtambule ametoa wito kwa vijana waendelee kuupenda mchezo wa ngumi kwa sababu ya kujenga uchumi wa nchi na kujipatia ajira.
Mkurugenzi wa Mafia Boxing, Ally Zayumba amesema Jumatatu Desemba 23, wanatarajia kuanza kupokea mabondia kutoka nje ambao wanakuja kucheza na wapinzani wao kutoka Tanzania.