Kriti atuhumiwa kutoka na mwanafunzi wa chuo

MUMBAI: Kriti Sanon amekuwa kwenye habari kuhusu penzi lake jipya na mfanyabiashara Kabir Bahia. Wanandoa hao wamekuwa wakisherehekea msimu wa sherehe pamoja, wakihudhuria harusi ya familia huko Dubai na kusherehekea Krismasi.
Walionekana pia kwenye tamasha la Ustad Rahat Fateh Ali Khan wikendi iliyopita. Hata hivyo mwanamtandao mmoja amemshtumu Kriti kwa kumlaghai mpenzi wake wa chuo akidai kuwa mwanafunzi mwenzake wa zamani.
Katika mazungumzo na YouTuber, Ranveer Allahbadia, Kriti Sanon alikana hilo lakini mwana mtandao huyo alidai katika maoni yake kwamba Kriti alienda Chuo Kikuu cha Jaypee na alikuwa na mpenzi wake ambaye ni tajiri aliwahi kumsaidia kifedha na pia alimsaidia kuhamia Mumbai, ambako waliishi pamoja, lakini baada ya kupata uhusika wake wa kwanza katika filamu, alibadilika na kumlaghai baada ya takriban miezi sita.
Dai hili la kushangaza limezua maswali, lakini mashabiki wengi wa Kriti hawaamini.
Mashabiki wengi wa Kriti Sanon wamemtetea kwenye mitandao ya kijamii, wakiita madai hayo ya uongo na utapeli.
“Shabiki mmoja alisema, “Mtu yeyote anaweza kutengeneza hadithi ya nasibu kwenye maoni ili kushambulia mtu. Nimeona maelfu ya maoni wakidai walienda shule au chuo chake. Mwingine alisema, “Hii ni fake; Ningeweza kuandika kitu kama hiki kwa urahisi nikidai kuwa rafiki yake au mpenzi wake wa zamani. Hii inaonekana kama mtu ambaye hampendi Kriti ndiyo ametengeneza thuma hizi.”
Sahabiki mwingine aliandika kwamba, “Sidhani kama Kriti alihitaji mpenzi tajiri; anatoka katika familia nzuri. Baba yake ni CA na mama yake ni profesa wa fizikia chuoni unafikiri kweli hakuwa na pesa?”
“Kriti hangefanya hivyo; ana moyo safi.” Baadhi ya watumiaji wa mtandao huo walipendekeza kwamba watu wanaompinga Kriti ndiyo wanaoeneza uvumi huo.”
Kwa upande wa kazi, Kriti Sanon alionekana mara ya mwisho kwenye filamu ya ‘Do Patti’, ambapo alicheza nafasi mbili pamoja na Kajol. Mwaka huu, pia ameigiza katika filamu nyingine mbili: ‘Teri Baaton Mein Aisa Uljha Jiya’, kichekesho cha mapenzi cha uongo cha kisayansi kilichomshirikisha Shahid Kapoor, na ‘Crew’, kichekesho kinachoongozwa na wanawake na Tabu na Kareena Kapoor Khan.