Nyumbani

Kocha Coastal Union aitwa baraza la wazee

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Coastal Union, David Ouma ameitwa na baraza la wazee wa timu hiyo mjini Tanga kwa ajili ya kujieleza kuhusu mwenendo mbaya wa timu hiyo.

Coastal Union hawakuwa na matokeo mazuri katika michuano ya CECAFA, Ngao ya Jamii na kupoteza mabao 3-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya F.C. Bravos do Maquis.

Akizungumza na Spotileo, Ofisa habari wa Coastal Union, Abass Elsabri amesema Alhamisi, Agosti 22 walifanya kikao kujadiliana mwenendo wa timu na Kocha wao Ouma kwenda Tanga kwa ajili ya kwenda kujieleza.

Coastal Union watakuwa wenyeji wa mchezo wa marudiano ya pili ya mkondo wa kwanza wa Afrika dhidi ya F.C. Bravos do Maquis ya Angola utakaochezwa, Jumapili, Agosti 25 uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini.

“Kwenye mechi yetu ya Jumapili, Agosti 25, Kocha wetu Ouma hatakuwa sehemu ya benchi la ufundi kwa sababu ya matokeo tuliyopata katika michezo ambayo tumecheza hivi karibuni,” amesema Abass.

Ameongeza kuwa nafasi ya Ouma kwa sasa itachukuliwa na kocha msaidizi Ngawina Ngawina akishirikiana na Joseph Lazaro katika mechi ya marudiano.

Amesisitiza kuwa kurejea kwa Ouma litakuwa suala na viongozi lakini wanaimani na makocha wazawa waliochukuwa nafasi yao kufanya vizuri katika mchezo huo wa marudiano.

Related Articles

Back to top button