Ligi KuuNyumbani

Che Malone afunguka kuichagua Simba

MLINZI mpya wa Klabu ya Simba Che Malone Fondoh amesema aliamua kujiunga na timu hiyo ili kuonesha daraja alilo nalo anapokuwa dimbani.

Che Malone amesema anafahamu Simba kuna wachezaji wenye ubora mkubwa hasa katika nafasi anayocheza lakini siku zote amekuwa ni mtu wa kufanya juhudi hivyo hana wasiwasi anaamini atapata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi cha miamba hiyo ya mitaa ya Msimbazi Dar es Salaam.

Malone ameongeza kwa kusema timu nyingi zilihitaji huduma yake lakini aliamua kuichagua Simba kutokana na klabu hiyo kuonesha nia ya dhati ya kuitaka huduma yake.

Kauli hizo za Mlinzi huyo wa kimataifa wa Cameroon amezitoa wakati akifanya mahojiano na Runinga ya mtandaoni ya klabu ya Simba.

Related Articles

Back to top button