Ligi Kuu

Hee! Yanga tena

DAR ES SALAAM: KLABU ya Yanga imekutana na rungu jingine la kufungiwa kusajili wachezaji wapya kwa msimu wa 2024/25 kutokana na kukiuka kanuni za usajili za FIFA.

Imeelezwa kuwa mchezaji anayeidai Yanga ni Hafiz Konkoni ambaye alivunjiwa mkataba wake kwenye dirisha dogo lililopita na nafasi yake kuchukuliwa na Joseph Guede.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), iliyotoka Juni 18, imevitaka vilabu vyote vinavyodaiwa na wachezaji wao kuwalipa haraka kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Yanga ni moja ya timu tano ambazo zimefungiwa na FIFA kusajili, ambapo tayari dirisha la usajili limefunguliwa tangu Juni 15, vilabu vingine ni Singida Fountain Gate FC, Tabora United, Biashara United na FGA Talents

Taarifa ya FIFA inakuja muda mfupi tangu Yanga ifungiwe tena kusajili mwezi Aprili kutokana na kutokamilisha usajili wa mchezaji wake kwenye mfumo wa usajili kwa njia ya Mtandao wa FIFA.

“Klabu itakayowalipa wahusika, itaondolewa mara moja adhabu ya kufungiwa kusajili, hadi leo asubuhi kupitia mfumo wa FIFA (FIFA Legal portal) hakuna taarifa ya klabu yoyote kati ya hizo iliyowalipa wahusika,” amesema Ofisa Habari wa TFF Cliford Ndimbo.

 

 

Related Articles

Back to top button