MasumbwiMichezo Mingine

Mandonga ajifagilia licha ya kupigwa

BONDIA Karim Mandonga amesema licha ya kupoteza pambano lake dhidi ya Daniel Wanyonyi bado anajivunia kuwa bondia mwenye ushawishi katika maeneo mbalimbali.

Mandonga amesema amepoteza pambano nchini Kenya lakini Wakenya wameendelea kutamani uwepo wake kwenye ardhi yao.

Bondia huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema Mungu akipanga jambo lake hakuna wakulizuia.

” Hata ukipanda tembele Mungu akipanga uvune dhahabu utavuna dhahabu, nipo na wadhamini kama wote ninatamba Nairobi.”amejinasibu Mandonga.

Mandonga alipoteza kwa alama za Majaji kwenye pambano hilo.

Related Articles

Back to top button