Ligi Kuu

JKT vs KMC ni pasua kichwa

DAR ES SALAAM: POINTI tatu ni jambo ambalo linawaumiza makocha wa timu ya JKT Tanzania na KMC FC,  kila mmoja anahitaji kuzisaka alama hizo kesho kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara Meja Jenerali Isamuhyo uliopo Mbweni.

Timu hizo zimekutana mara sita na kutoka sare mechi mbili. JKT Tanzania walishinda mechi mmoja kati ya michezo mitatu waliocheza nyumbani na kushindwa kupata matokeo ugenini, KMC FC imeshinda michezo mitatu, wanapata changamoto ya kutopata matokeo ugenini na kushinda nyumbani mara tatu na kupoteza ugenini.

Kuelekea mchezo huo Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Ahmad Ally amesema ameandaa kikosi chake kulingana na ubora wa KMC FC na anaimani ya kupata pointi tatu nyumbani.

“Hatuangalii matokeo ya nyuma ya mpinzani wetu, tumejaribu kuangalia pande zote mbili ubora wa washambuliaji na ulinzi, nina imani tutatengeneza nafasi ya kupata pointi tatu,” amesema Kocha huyo.

Kocha wa KMC FC, John Matambala amesema baada ya kupoteza mechi iliyopita kwa idadi kubwa ya kubwa ya mabao mbele ya Azam FC, kufanyia kazi mapungufu safu ya ulinzi na mabadiliko yapo kwenye mechi ya kesho.

“Tutacheza kwa tahadhari kubwa dhidi ya JKT Tanzania, mpango kazi mkubwa wa kutafuta matokeo kwenye mchezo wetu wa kesho, tumefanyia kazi makosa yaliyokea kwa ajili ya kupata matokeo kwenye mechi hii,” amesema John.

Related Articles

Back to top button