kiza kinene!

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Simba Fadlu Davids amekiri kuwa ana kazi kubwa ya kuchangua kipa namba mmoja kati ya Aishi Manula na Moussa Camara ndani ya kikosi cha kwanza.
Kauli hiyo ya Fadlu ni baada ya makipa wa Simba, Manula na Camara kufanya vizuri katika timu zao za Taifa kwenye michuano ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (AFCON ) ambapo Stars imefuzu.
Kocha huyo alikuwepo uwanja wa Benjamin Mkapa akishuhudia mechi ya AFCON kati ya Taifa Stars dhidi ya Guinea ambapo akiangalia wachezaji wake akiwemo makipa hao, Manula na Camara.
Manula ambaye alidakia Taifa Stars ambayo iliibuka na ushindi wa bao 1-0 huku Camara akiwa katika Taifa lake la Guinea katika mchezo wa kundi H.
Fadlu amesema ni jambo la furaha kuona makipa hao wakifanya vizuri katika timu zao na kuendelea kuumiza kichwa kutokana na ubora wa Manura na Camara.
“Kurejea kwa kiwango cha Manula kuna kwenda kuongeza ushindani mkubwa ndani ya kikosi cha Simba, ameonyesha ukubwa wake katika mechi ngumu iliyokuwa ikibeba hatma ya Stars kutinga AFCON.
Ninafahamua nina makipa wengi lakini ujio wangu uwanjani umeniongezea kitu cha kufanyia kazi na nimeweza kuwasoma wachezaji wangu kwa upana zaidi,” amesema Fadlu.
Camara amefanikiwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Fadlu kwa kucheza mechi 10 za ligi huku Ally Salim alionekana katika mechi moja ya kirafiki.