Africa

Kocha Mamelod anyolewa

Mamelodi Sundowns wamethibitisha kuachana na kocha mkuu Rhulani Mokwena.

“Sundowns inapenda kutoa shukurani zake kwa Rhulani Mokwena kwa mchango wake katika mafanikio na mafanikio ya klabu katika kipindi chake kama kocha mkuu,” imeeleza taarifa hayo.

Taarifa ya Mamelod imeeleza kuwa kocha huyo atakuwa sehemu ya familia ya timu hiyo na klabu inamtakia kila la heri.

“Uamuzi wa Mamelodi Sundowns ulichukuliwa na Bodi kwa kuzingatia malengo na matarajio ya Klabu na haukushawishiwa au kulingana na mapendekezo ya mtu yeyote anayehusishwa na klabu,” imefafanua taarifa hiyo.

Aidha kocha Manqoba Mngqithi na timu ya ufundi wataendelea kuongoza na kudhibiti mazoezi na maandalizi ya wachezaji kwa ajili ya msimu ujao, imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button