Kikapu

Fox Divas, Vijana Queens waendelea kutetea taifa kikapu Afrika

ZANZIBAR:FOX Divas ya Mara mambo sio shwari baada ya kupoteza mchezo wa tatu leo dhidi ya Equity benki ya Kenya katika mchezo wa kufuzu Ligi ya Kikapu Afrika kwa wanawake kanda ya mashariki (WBLA) kwa pointi 48-87 kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.

Wageni walimiliki mpira katika robo tatu ya mchezo huo kwa pointi 22-31, 36-49 na 43-69 kisha ushindi huo wa jumla ya pointi 48-87 katika robo ya nne na mwisho.

Kabla ya mchezo, walipoteza jana dhidi ya Gladiators ya Burundi kwa pointi 77-67.

Gladiators ilimiliki mchezo kwa robo tatu kwa pointi 24-12, 38-35 na robo ya nne 77-67 huku robo ya tatu wakitoka sare kwa pointi 57-57.

Mchezo wa ufunguzi Fox Divas ilipoteza kwa pointi 105-45 dhidi ya REG ya Rwanda.

Mwakilishi mwingine wa Tanzania ni Vijana Queens ya Dar es Salaam iliyopoteza mchezo dhidi ya Al Ahly ya Misri jana kwa pointi 145-52.

Katika robo ya kwanza Al Ahly iliongoza katika robo zote nne za mchezo huo kwa pointi 28-12, 62-23, 112-37 na mwisho 145-52.

Mchezo wa kwanza Vijana Queens walishinda kwa pointi 91-77 dhidi ya Young Sisters ya Burundi. Vijana iliongoza robo tatu ya mchezo. Ilipoteza robo ya kwanza 24-26 ikarudi kwenye mchezo na kufanya vizuri robo tatu zilizobaki pointi 44-42, 69-61 na 91-73.

Vijana Queens itacheza mchezo mwingine leo jioni dhidi ya J.K.L Ladies ya Uganda

Related Articles

Back to top button