Kwingineko
Hii timu inagawa dozi bila kuangalia usoni

TIMU ya taifa ya Mexico imeonesha kuwa ni moja ya timu zinazopaswa kuogopwa katika Kombe la Dunia 2026 baada ya kutawala Kundi A na kumaliza hatua ya makundi kwa ushindi wa mechi zote tatu.
Ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya taifa ya Czechia uliihakikishia Mexico kumaliza kileleni mwa kundi hilo, huku ikikusanya alama zote tisa zilizokuwa zinapatikana.
Kiwango hicho kimeifanya Mexico kuwa moja ya timu zilizovutia zaidi katika hatua ya makundi, huku safu yao ya ushambuliaji na ulinzi vikionesha uthabiti mkubwa.
Kwa upande wa Czech, matokeo hayo yamehitimisha safari yao katika Kombe la Dunia 2026 baada ya kushindwa kupata matokeo yaliyoweza kuwapa nafasi ya kuendelea.
Mbali na kutinga hatua ya 32 bora, Mexico pia imepata faida nyingine muhimu kwani mechi zake za hatua ya mtoano zinatarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Azteca, moja ya viwanja maarufu zaidi duniani na nyumbani kwa mashabiki wao.
Mashabiki wa Mexico sasa wanaanza kuota ndoto za kuona timu yao ikienda mbali zaidi katika mashindano haya, hasa kutokana na kiwango bora walichoonesha tangu mwanzo wa michuano.




