Muziki

Gigy na Ali Kiba mbona fresh tu!

DAR ES SALAAM: Msanii wa Bongo fleva nchini Gift Stanford ‘Gigy Money’ amesema kuwa hana tofauti yoyote na msanii mwenzake Ali Kiba wanapendana na kushirikiana katika kazi zao.

Gigy Money amesema kuwa hajawahi kuwa na ‘bifu’ na Ali Kiba anachokisemaga kwa watu huwa anawaigizia lakini wanapendana.

“Ali kiba ni mtu poa sana ananipenda ninampenda tunapendana wote ni wasanii tunashirikiana kwanye kazi akinionaga sehemu yoyote huwa anacheka tu mwenyewe tunajuana.

“Hayo mnayoyazusha nyie waandishi ndio anawaigizia hatuna tofauti hatujawai kugombana tuko poa kiroho safi kazi zinaendelea.’

Gigy Money ameongeza kuwa anawapenda wasanii wote wa bongo hana shida na yoyote yule labda mtu ndio aweke bifu na yeye lakini kwa upande wake hana bifu na mtu anabifu na njaa.

Related Articles

Back to top button