Rema aachia albamu ya pili aliyoipa jina ‘HEIS’

LAGOS: YOTA wa muziki wa Nigeria Divine Ikubor maarufu kwa jina la Rema ametoa albamu yake ya pili inayoitwa, ‘HEIS’.
Albamu hii inaonyesha mchanganyiko wa kipaji na usanii wake ambapo amechanganya aina mbalimbali za muziki wenye ubunifu na sauti tofauti zitakazowavutia mashabiki wake watakaosikiliza albamu hiyo.
Albamu ya ‘HEIS’ inamuonyesha Rema akiwa na hali ya kurudisha utawala wake wa muziki na kuwaaminisha wanigeria kwamba naye ni miongoni mwa wasanii wenye mafanikio makubwa kwa ndani nan je ya Nigeria kama Wiz Kid, Davido na Burna Boy.
“Afrika, Nigeria, na Benin City ndizo mada kuu zinazounganisha mradi huu ambao ‘HEIS’ inaelezea utamaduni, ukuaji na mafanikio ya Rema,” alisema Rema.
Albamu yake ya ‘Rave & Roses Ultra’, ilikuwa na wimbo uliopata umaarufu mkubwa ‘Charm’ ambao uliweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa Kiafrika kuvuka wafuatiliaji bilioni1 kwenye mtandao wa Spotify. Rema ameshinda tuzo ya VMA akiwa msanii wa kwanza mwafrika kushinda tuzo ya wimbo bora pia amekuwa msanii wakiafrika aliyeshika chati kwa muda mrefu zaidi kwenye Billboard Top 100.
Na mafanikio yake yalimfanya kuingia kwenye Kitabu cha rekodi cha Guinness kwa kushika nafasi ya kwanza kwenye MENA. chati. Miongoni mwa vibao vyake vilivyoongoza chati ni ‘Calm Down’ iliibuka kama wimbo wa mwaka 2023, na kupanda hadi nambari 4 kwenye Chati Rasmi za Uingereza na Nambari 5 kwenye Billboard Hot 100 na kupata vyeti vya dhahabu na almasi