Burudani

Gekul ataka wasanii wapate mikopo

Naibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul amewaagiza maafisa utamaduni nchini kusimamia vyema Mfuko wa Utamaduni na Sanaa katika ngazi za mikoa na halmashauri ili kuhakikisha wasanii walioko katika maeneo yao wanapata mikopo kupitia mfuko huo.

Gekul ametoa agizo hilo leo jijini Dodoma wakati akifungua Kikao Kazi Cha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Maafisa Utamaduni Tanzania Bara.

Naibu Waziri amesisitiza maafisa hao kuongeza juhudi katika kusimamia shughuli za Utamaduni na Sanaa katika maeneo yao.

Related Articles

Back to top button