Tennis
Gauff atinga raundi 3 French Open

Mchezaji tenisi wa kimarekani Coco Gauff ametinga raundi ya 3 ya Roland Garros alipomshinda Tamara Zidansek wa Slovenia.
Gauff amemshinda kwa urahisi Zidansek kwa seti 6-3 6-4 katika mzunguko wa pili mbele ya umati wa watu waliokuwa wakimshangilia.
Kwa ushindi huo, sasa Gauff atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Wang Yafan wa China na Dayana Yastremska wa Ukraine.
“Nimefurahi sana na jinsi nilivyocheza. Hali ya hewa haikuwa nzuri lakini nimeweza kuishinda,” amesema Gauff.
Mapema wakati wa mchezo Gauff anayeshika namba 3 duniani kwa ubora kwa mchezaji mmoja mmoja alipata upinzani toka kwa mwanafainali wa zamani, Zidansek.