Fadlu:Kesho ni pira ubaya ubwela

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amesema wachezaji wake wapo tayari kwa mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahly Tripoli kutokana na maandalizi waliyofanya na wanahitaji ushindi.
Simba kesho wana kibarua kigumu cha kusaka ushindi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam kwa ajili ya kutafuta kufuzu hatua ya makundi ya Kombe Shirikisho Afrika.
Kocha Fadlu amesema wachezaji wake wapo tayari na wamewekeza zaidi katika kutafuta ushindi dhidi ya Al Ahly Tripoli ya Libya kwa kutafuta nafasi ya kusonga mbele katika mashindano hayo.
“Mechi iliyopita ilikuwa ya ushindani mkubwa na ana imani mchezo wa kesho hautakuwa rahisi kwa sababu kila mmoja ana nafasi ya kusomga mbele, lakini wao wanahitaji zaidi kufuzu makundi,” amesema Fadlu.
Nahodha wa Simba Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr ‘, amesema maandalizi yameenda vizuri leo wanamalizia mazoezi ya mwisho ya kumkabili mpinzani wao Al Ahly Tripoli.
Amesema kesho ni mchezo muhimu sana, wachezaji wamepata muda wa kuzungumza na kuangalia baadhi ya mechi kama hizo ambazo wanahitaji kufuzu makundi.
“Tuna deni kubwa sana la kurudisha imani kwa wanasimba, ukizingatia hatujafanya vizuri sana lakini kesho ni sehemu yetu ya kufanya kile kinachotarajiwa na wanasimba, amesema mchezaji huyo.