RAIS Samia Suluhu Hassan ameagiza maandalizi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) 2027 zitakazoandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Uganda na Kenya yafanyike kikamilifu.
Ametoa maagizo hayo wakati akishukuru na kutoa pongezi kwa wote waliohakikisha Tanzania inapata fursa hiyo.
“Nawaagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha tunafanya maandalizi mazuri, ikiwemo kukamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu, viwanja viwili vipya vya kisasa vya michezo Arusha na Dodoma,” amesema Samia.
Fainali za AFCON 2023 zitafanyika Ivory Coast mwaka 2024 wakati Morocco itaandaa fainali za mwaka 2025.