Diamond, Zuchu: Sandra ataamua mwenyewe

DAR ES SALAAM: MSANII wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, na msanii Zuchu wamezungumzia uwezekano wa mtoto wao Sandra kuingia kwenye muziki endapo atakuwa na shauku ya kufanya hivyo.
Wawili hao waliulizwa iwapo, kwa kuwa wao ni wasanii, watamruhusu Sandra kufuata nyayo zao na kuwa msanii.
Akijibu swali hilo, Diamond alisema bado ni mapema kutoa uamuzi kuhusu jambo hilo.
“Aaah, sijajua, ni mapema sana kusema hivyo,” alisema Diamond.
Kwa upande wake, Zuchu alitoa jibu lenye kuacha nafasi kwa Sandra kuamua mwenyewe, akisema atamruhusu iwapo atakuwa na tabia zinazofanana na zake.
“Kama atakuwa na tabia kama zangu, nitamruhusu,” amesema Zuchu.
Katika mahojiano hayo, Diamond pia amezungumzia jinsi baadhi ya watoto wake wanavyofanana, akisema familia yao imebarikiwa na Mwenyezi Mungu kwa kuwapa watoto wenye sura zinazofanana na wazazi na ndugu zao.
Diamond Platnumz amesema hata ukiwaangalia Tossy na Ricardo Momo, wanafanana kwa kiasi kikubwa na watoto wao.
Hata hivyo, mahojiano hayo yalipata burudani zaidi baada ya mtoto wao Nillan kuingilia mazungumzo na kumuomba baba yake apewe kipaza sauti ili naye aweze kuzungumza.




