Mastaa

Diamond akerwa na tabia za Chris Brown

NEW YORK: ALIYEKUWA mpenzi wa Chris Brown na mama wa mtoto wake, Diamond Brown, anadai kuwa mwanamuziki huyo anatoa vitisho kwa wapenzi wake wapya, akitaka hilo likomeshwe mara moja.

Hayo yameelezwa kupitia makabrasha ya nyaraka zilizowasilishwa katika mzozo wao mkali kuhusu malezi ya mtoto.

Diamond alisema uhusiano wake na Chris uliisha miaka miwili iliyopita na licha ya Chris kuwa na mpenzi mpya, ambaye amezaa naye mtoto, yeye hukasirika sana anapoanza uhusiano na wanaume wengine tangu walipoachana.

“Ametoa vitisho vya kifo dhidi ya mpenzi wangu wa hivi karibuni, alifanya hivyo pia kwa mwanaume mwingine niliyeanza kuwa naye takriban miaka miwili iliyopita baada ya mimi na yeye kuachana,” alidai Diamond.

“Mahusiano haya yote mawili yalivunjika kwa sababu ya tabia ya Chris ya kunisumbua na kuninyanyasa. Sipaswi kuishi kwa hofu ya kuendelea na maisha yangu kwa sababu ya hasira na chuki ya Chris.

“Sijachukua hatua yoyote hadi sasa, lakini nimemuomba wakili wake, tangu mwezi Machi, kupitia wakili wangu, ili Chris aache tabia hii,” alifafanua Diamond.

Diamond pia anabainisha kuwa Chris ambaye anaamini ana utajiri wa Dola milioni 50 anaingiza kipato kikubwa zaidi ikilinganishwa na yeye anayepata Dola 1,500 kwa mwezi lakini bado anakataa kutoa mchango wa kutosha kwa ajili ya matunzo ya binti yao, Lovely.

Imeelezwa Chris amekanusha madai ya Diamond ya unyanyasaji kupitia barua pepe inayodaiwa kutoka kwa wakili wake kwenda timu ya Diamond.

Aidha, Diamond alimshtaki Chris kuhusu malezi ya mtoto Mei, mwaka huu. Aliomba malezi ya awali, jambo ambalo Chris alilipinga pia.

Related Articles

Back to top button