Kwingineko

Deschamps: Mbappe anarudi

PARIS: KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps amesema nahodha wa kikosi hicho na mshambuliaji kinara Kylian Mbappe atarejea kwenye kikosi cha timu ya taifa katika mechi za robo fainali ya UEFA Nations League dhidi ya Croatia mwezi ujao.

Mbappe aliyeichezea Ufaransa michezo 86 hajawa sehemu ya kikosi hicho tangu alipojiunga na Real Madrid mwezi Julai mwaka jana akizikosa mechi za Nations League za Oktoba na Novemba.

Deschamps ameliambia gazeti la L’Equipe la nchini humo kuwa anafikiria kumjumuisha mshambuliaji huyo hatari wa Real Madrid kwa michezo hiyo ya robo fainali.

“Atakuwepo, kwanini asiwepo? Kama atajituza na atabaki na kiwango alichonacho nafikiria kumrejesha kikosini, ana uhusiano mzuri sana na timu ya taifa. Hata kama amekuwa na kipindi kigumu lakini kila mtu sasa anaona amerejea kwenye kiwango chake cha kawaida” – Amesema Deschamps

Ratiba ya soka kwa siku za hivi karibuni imekuwa mfupa mgumu kwa wachezaji kote ulimwenguni huku yakisikika malalamiko ya ugumu huo kuongeza namba ya majeruhi kwenye vikosi, hata hivyo Mbappe alisema mwezi Desemba kuwa bado anaipenda timu hiyo licha ya kuachwa nje ya kikosi.

Related Articles

Back to top button