Riadha

CRDB yatenga Sh milioni 120 za Marathon

DAR ES SALAAM: BENKI ya CRDB imetenga zaidi ya Sh milioni 120 kwa washindi watakaoshinda mbio za marathon zitakazofanyika Agosti 16 Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na mgeni rasmi Waziri Mkuu Dk Mwigulu Nchemba.

Aidha, fedha nyingi za zawadi zitatoka kwa mshindi wa km 42 ambaye ataondoka n ash milioni 12 huku washindi wengine wa pili mpaka sita nao wakitarajiwa kuondoka na fedha kwa viwango tofauti. Mbio nyingine zenye fedha nyingi ni km 21 ambapo mshindi ataondoka na milioni sit ana pia kutakuwa na mbio za baiskeli za km 65 zenye zawadi nono.

Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB benki Foundation Tully Easter Mwambapa amesema lengo la mbio hizo ni kuhamasisha Watanzania kufanya mazoezi, kujenga afya ya mwili na akili, pamoja na kuwaunganisha watu kupitia michezo na burudani.

“Maandalizi yam bio hizi yamefikia hatua kubwa na asilimia 89 ya lengo la ushiriki likiwa tayari limefikiwa. Tunaendelea kuwahimiza watu kujitokeza kwa wingi kwani tutakuwa na washiriki kutoka ukanda wa Afrika Mashariki,”amesema.

Amesema: “Tumetenga zawadi za zaidi ya Sh milioni 120. Hakuna mdau mwingine Tanzania ambaye amewahi kutenga kiwango hicho kikubwa cha fedha ,”.

Mbio hizo zitahusisha pia kilomita tano na 10 kwa wakimbiaji na watembeaji, huku CRDB ikisema njia zote zimefanyiwa majaribio na kuthibitishwa kwa kushirikiana na kampuni za kimataifa zenye utaalamu wa kusimamia mazingira ya marathon.

Kwa upande wa usalama, CRDB imesema inashirikiana na Jeshi la Polisi na wadau wengine kuhakikisha washiriki na watazamaji wanakuwa salama katika maeneo yote ya mbio.

Kwa mujibu wa Mwambapa, mbio hizo zimeendelea kupata mwitikio kutoka ndani na nje ya Tanzania, ikiwamo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burundi, ambako shughuli zinazohusiana na marathon zimefanyika.

Related Articles

Back to top button