Ligi Kuu

Bocco akiwasha, JKT ikiikazia Azam

TIMU ya JKT Tanzania imeibana mbavu Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa leo Agosti 28 Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo huku mshambuliaji mpya wa JKT John Bocco akicheza mchezo wake wa kwanza.

Katika mchezo huo Bocco alikuwa akisubiriwa kwa hamu na mashabiki ameingia dakika ya 89 akichukuwa nafasi ya Charles Ilanfya .

Dakika 45 kipindi cha kwanza JKT Tanzania, ilimiliki mpira na kutengeneza nafasi nyingi lakini walishindwa kuzitumia huku Azam FC wakizinduka dakika za mwisho za mchezo.

Wachezaji wa Azam FC walianza mechi kwa morali ya chini, tofauti na JKT Tanzania iliyokuwa inatumia nguvu na kasi kusaka bao, ingawa umaliziaji haukuwa mzuri, safu ya ushambuliaji iliongozwa na Edward Songo, Ismail Aziz Kada na Najim Magulu.

Kwa upande wa Azam FC, Fei Toto na Gibril Sillah walijikuta wanafanya kazi kubwa ya kushuka chini kutafuta mipira walijikuta wanakumbana na ugumu wa kunyang’anywa mipira kabla ya kufika eneo la kipa wa JKT .

Related Articles

Back to top button