Nyumbani

Kivumbi Ligi ya Championship leo

PATASHIKA ya Ligi ya Championship inaendelea leo kwa michezo mitatu kufanyika Mbeya, Mwanza na Arusha.

Huko Nyanda za Juu Kusini, kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, wenyeji Mbeya City itaikaribisha Stand United ya Shinyanga.

Green Warriors ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa TMA kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Miamba ya zamani ya Kanda ya Ziwa, Pamba ambayo sasa inaitwa Pamba Jiji itakuwa uwanja wa nyumbani wa Nyamagana kuikabili Mbeya Kwanza.

Related Articles

Back to top button