Tetesi
Barcelona yakomaa na Gundogan
NAHODHA wa Manchester City, Ilkay Gundogan yuko mbioni kujiunga na Barcelona mkataba wake utakapokamilika msimu huu wa joto.
Imeripotiwa klabu hiyo ya La Liga inaendelea kumshawishi kiungo huyo wa kati wa Ujerumani, 32, kwa ofa ya mkataba wa miaka mitatu. Mtandao wa umeeleza.
Taarifa zinasema kuwa Gundogan pia anawania na Arsenal, kinachosubiriwa ni kukamilika kwa msimu huu, ili kuanza mazungumzo.
Bado haijawekwa wazi kama nyota huyo ataendelea kusalia City kwa kuongeza mkataba au ataondoka kusaka maisha mengine.