Ligi Kuu

Azam waleeeeeeee!

DAR ES SALAAM: AZAM FC imekusanya alama tatu baada ya kuwatandika walima alizeti Singida Black Stars mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika muda mchache uliopita.

Mabao ya Azam kwenye mchezo huo yamefungwa na Feisal Salum dakika ya 38 na Jhonier Blanco 57′ huku bao la Singida Black Stars likifungwa na Elvis Rupia dakika ya 62 ya mchezo.

Matokeo hayo yameifanya Azam FC kufikisha pointi 27 katika nafasi ya 2 pointi moja nyuma ya vinara wa ligi Simba wenye pointi 28. Singida Black Stars wao wanasalia nafasi ya 4 wakiwa na pointi 24 nyuma ya Yanga wanaokamata nafasi ya tatu wakiwa na pointi 24.

Huu unakuwa mchezo wa nne mfululizo wa Black Stars bila ushindi licha ya kuanza ligi kwa kishindo kikubwa ila sasa ni kama bundi wa kukosa matokeo ametawala viunga vyao.

Kwa upande wa Azam FC ni kama kocha Rachid Taousi ameupata ufunguo kwani wanaendelea kugawa dozi kwa kila anayekatiza anga zao.

Related Articles

Back to top button