Albamu mpya ya Darasa ina mawe balaa!

DAR ES SALAAM: MSANII wa Bongo Fleva Shariff Ramadhan maarufu Darasa Februari 7 mwaka huu wa 2025 ataachia albamu yake mpya aliyoiita ‘Take Away the Pain’.
Albamu hiyo ina jumla ya nyimbo 15 zikiwemo alizoshirikisha wasanii wengine wenye majina makubwa katika muziki afrika.
Darasa anayetamba na wimbo wa ‘Mind Your Business’, ‘Too Much’, ‘I Like It’, na ‘Loyalty’ amewataja wasanii watakaosikika katika albamu hiyo ni Alikiba, Harmonize, Mbosso, Zuchu, Bien, Jay Melody na Jovial.
Ameendelea kuzitaja baadhi ya nyimbo zitakazokuwepo katika albamu hiyo ni pamoja na wimbo maarufu wa ‘Mazoea’ aliomshirikisha Harmonize, ‘Romeo’ aliomshirikisha Zuchu na ‘Looking For Love’ aliomshirikisha Mbosso.
Darassa ameshukuru mashabiki wake kumsapoti kwa muda wote aliokuwa akifanya muziki wake na kutoa nyimbo mbalimbali.
Albamu hiyo imeandaliwa na maprodyuza mahiri katika soko la muziki ndani na nje ya Tanzania akiwemo Kaniba Creator, Kapipo Beats, Blvcq Igbo6, FoxxMadeIt, Trone, S2Kizzy na Abbah.
Darasa ni mmoja wa marapa na watunzi wa nyimbo wenye ushawishi mkubwa nchini Tanzania. Alipata umaarufu mkubwa kwa mara ya kwanza kwa wimbo wake wa ‘Muziki’ aliomshirikisha Ben Pol, ambao ulikuja kuwa wimbo bora sana Afrika Mashariki na Kati.