Burudani
Wolper hataki tabu
Msanii wa Bongo Movie nchini Jackquline Wolper amesema hakuna ugomvi mtakaosikia kutoka kwake Wema Sepetu, Irene Uwoya, Elizabeth Michael na Kajala.
Akizungumza na waandishi wa habari Wolper amesema zamani ilikuwa utoto saivi wameshakuwa watu wazima.
“Hakuna ugomvi utausikia kutoka kwa top 6 Wema, Kajala, Anty Ezekiel na Irene Uwoya ilikuwa utoto saiv sisi niwatu wazima tuna watoto hatufanyi ujinga.”
Aidha amesema kuwa mtashuhudia mambo makubwa kutoka kwa Top 6, ni kazi kwa kwenda mbele.