Tetesi

Mbio kumsajili Mbappé zahamia EPL

TETESI za usajili zinaonesha Chelsea, Liverpool, Manchester United na Newcastle United zinazoshiriki Ligi Kuu England (EPL) zinaweza kutoa ofa ya kumsajili fowadi wa kifaransa Kylian Mbappé baada ya ripoti kwamba Real Madrid haina mpango kumsajili.

Mbappé ataingia miezi sita ya mwisho ya mkataba wake Paris Saint-Germain Januari 2024. (FourFourTwo)

Tottenham inapanga kumsajili beki wa kati wa kushoto Januari 2024 baada ya kugundua kiwango cha jeraha la Micky van de Ven huku beki wa England anayekipiga Bournemouth, Lloyd Kelly, mwenye umri wa miaka 25 akiwa kipaumbele.(Standard)

Maskauti wa Arsenal wamesafiri hadi Hispania kumshuhudia kiungo wa Real Sociedad, mhispania Martin Zubimendi mwenye umri wa miaka 24 wakati klabu yake ikicheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi Benfica. (90min)

Manchester United inatarajiwa kuwasiliana na FC Porto kuhusu uhamisho wa mshambuliaji mzoefu wa Iran, Mehdi Taremi mwenye umri wa miaka 31 ambaye anaweza kupatikana kwa ada ya Euro milioni 10.(Teamtalk)

Related Articles

Back to top button