Tetesi
Barcelona wamtaka Cancelo, Silva

Barcelona wanapanga kuwachukua kwa mkopo wachezaji Joao Cancelo, 29, na Bernardo Silva, 28 kutoka Man City.
Imeelezwa klabu hiyo iko tayari kuwanunua msimu ujao.
Wiki iliyopita, kocha wa Manchester City, Pep Guardiola alisema kama Barca wanahitaji huduma ya Bernado basi wafike Manchester waanze mazungumzo na kufuata taratibu zinazotakiwa.
Cancelo bado hajapata uhakika wa kucheza City, msimu uliopita alipelekwa Bayern Munchen kwa mkopo wa msimu mmoja na sasa amerejea akiwa hana uhakika wa nafasi ya kucheza.