Kane aitaka Bayern

Harry Kane anataka kujiunga na Bayern Munich baada ya kufanya mazungumzo kuhusu vipengele binafsi na bingwa huyo wa Ujerumani ambayo inashinikiza kukubaliana na Tottenham Hotspur kuhusu ada ya mshambuliaji huyo.
Bayern iliimarisha nia yake kwa Kane baada ya kuwasilisha ombi la ufunguzi la pauni milioni 60 sawa na shilingi bilioni 178.9 pamoja na nyongeza ambayo imechukuliwa kuwa ya chini sana na litahitajika kufikia angalau pauni milioni 100 sawa na shilingi bilioni 298 kujaribu kufanikisha dili hilo.
Hata hivyo, mkataba wa Kane unamalizika msimu ujao na ameonesha dalili ndogo ya kutaka kusaini nyongeza hivyo kuhatarisha Spurs kumpoteza kwa uhamisho huru.
Kutokuwepo kwa uhakika kuhusu mkataba wa Kane kunaweza kuongeza nafasi ya Bayern na itakuwa jambo la kuzingatiwa kwa mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy, anapojiandaa kwa mapambano ya kumbakisha mchezaji huyo.
Kumekuwa na hisia kwamba Spurs huenda ikakataa ofa yoyote ya kumsajili Kane majira haya ya joto na inasubiriwa kuona iwapo Bayern ina nia kutoa zaidi ya pauni milioni 100.
Kikwazo ambacho kinaweza kuikumba Bayern ni kusita kwa Kane kuondoka England.
Aidha kwa muda mrefu Manchester United imekuwa na nia kumsajili Kane lakini imeshindwa kukamilisha dili kutokana na uthamini wa Spurs wa mshambuliaji huyo.
Real Madrid pia inafirikiwa kutaka kumsajili Kane tangu ilipompoteza Karim Benzema aliyehamia Al-Ittihad ya Saudi Arabia lakini nguvu ya nia hiyo huenda ikategemea iwapo inaweza kumsajili Kylian Mbappé wa Paris Saint-Germain.
Kane amefunga magoli 41 kwa Klabu na England msimu uliopita.