Filamu

Dullvan afika maisha yake halisi kwenye filamu ya ukweni

DAR ES SALAAM: MSANII wa Ucheshi nchini, Abdallah Sultan ‘Dullvani’, amefichua kuwa filamu yake mpya ya Ukweni imebeba sehemu kubwa ya simulizi za maisha yake halisi, ikiwamo changamoto alizowahi kukutana nazo katika mahusiano na namna baadhi ya watu wanavyodharau kazi ya uchekeshaji.

Dullvani ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa filamu, ilizinduliwa katika Ukumbi wa EACLC, Ubungo jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia Dullvan amesema maudhui ya filamu hiyo, ameamua kutumia baadhi ya matukio aliyopitia katika maisha yake kama sehemu ya kujenga simulizi itakayowafanya watazamaji kutafakari mambo mbalimbali yanayotokea katika jamii.

Amesema miongoni mwa matukio yaliyompa msukumo ni changamoto alizowahi kukutana nazo katika mahusiano yake, ikiwamo siku alipokutana na mama wa aliyekuwa mpenzi wake na kupata mwitikio uliomfanya kutafakari namna jamii inavyowachukulia wachekeshaji.

Kwa mujibu wa Dullvani, “Kuna dhana kwa baadhi ya watu kuwa kazi ya uchekeshaji si kazi inayopaswa kuchukuliwa kwa uzito, jambo ambalo linaweza kuwaumiza wasanii wanaojituma katika tasnia hiyo.

Ameeleza kuwa “Kupitia filamu hii, nimegusa pia changamoto za mapenzi na namna matukio mbalimbali ya maisha yanavyoweza kuwa sehemu ya kujifunza na kujenga mtazamo mpya”.

Uzinduzi wa Ukweni unaashiria hatua nyingine katika safari yake ya kisanii, akionyesha kuwa uwezo wake hauishii katika kuchekesha pekee bali pia kuwasilisha simulizi zenye kugusa maisha ya watu.

Filamu hiyo inapatikana kupitia mtandao wa Paoflix.Kwa kazi hiyo, Dullvani anaonyesha namna uzoefu wa maisha unavyoweza kuwa sehemu muhimu ya ubunifu katika tasnia ya filamu nchini.

Kwa upande wake Mwongoza filamu hiyo Siamon Cheleani amesema kubwa Ukweni ni filamu bora iliyorekodiwa hapa Tanzania ukiangalia utashika kutazama ni kazi nzuri yenye viwango.

Related Articles

Back to top button