EPLKwingineko

Chelsea, Liverpool kumgombea Nunes

KLABU za Chelsea na Liverpool zinatarajiwa kugombea saini ya Matheus Nunes wa Wolverhampton Wanderers majira yajayo ya joto.

Timu hizo zikitaka kuimarisha eneo la kiungo kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Ureno anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 44 sawa na shilingi bilioni 125.6.

Ripoti zimesema Kocha wa Chelsea Graham Potter anatarajiwa kuanza kutowategemea N’Golo Kante na Jorginho ambao wana zaidi ya miaka 30 huku Nunes akitajwa kuwa mmoja wa walengwa kwenye safu ya kiungo.

Chelsea inavutiwa na Nunes mwenye umri wa miaka 24 na inaarajiwa kuingia kwenye mbio za kumsajili mwisho wa msimu atakapoingia sokoni baad aya msimu mmoja tu klabu ya Wolves.

Nunes yupo katika orodha ya wachezaji wanaowaniwa na Cheslea wakiwemo nahodha wa West Ham Declan Rice, Moises Caicedo wa Brighton na Amadou Onana wa Everton.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button