Charlene Ruto: Nilidhani nitaolewa na Mkenya, Mungu akanipa wa Mwanza, Tanzania

MWANZA: MTOTO wa Rais wa Kenya, William Ruto, Charlene Ruto, amegusa hisia za waumini baada ya kueleza namna alivyomuomba Mungu amjaalie mume mwenye upendo na hofu ya Mungu, lakini hakutarajia angeolewa na mwanaume kutoka Mwanza, Tanzania.
Charlene ameeleza hayo alipohudhuria ibada ya Jumapili, Novemba 8, 2026, jijini Mwanza, akiwa pamoja na mumewe, Isaya Yunge, siku chache baada ya kufunga ndoa.
Akizungumza mbele ya waumini, Charlene amesema “Awali nilikuwa nikidhani angeolewa na mwanaume kutoka nchini Kenya, lakini Mungu alikuwa na mpango tofauti na maisha yangu kwa kumleta Isaya, ambaye amesema ana sifa zote nilizokuwa akiziombea.
Amesema ” Moja ya mambo niliyokuwa nikimuomba Mungu ni kumpata mwanaume mwenye upendo na anayemcha Mungu, nimefurahi kuona maombi yangu yakijibiwa kupitia ndoa yangu na Isaya.
Katika tukio hilo, Charlene pia amewashukuru wakazi wa Mwanza kwa mchango wao katika kumlea na kumkuza mumewe hadi kufikia hatua ya kukutana naye na hatimaye kufunga ndoa.
Ujumbe wake uliambatana na hisia za furaha huku akionekana kutoa machozi wakati akieleza namna anavyomshukuru Mungu kwa hatua hiyo mpya ya maisha yake.
Mumewe, Isaya, aliyekuwa pembeni yake, alionekana kumfuta machozi kwa upendo, tukio lililovuta hisia za waumini na kuzua maoni mbalimbali kutoka kwa watu waliofuatilia video hiyo mitandaoni.
Baadhi ya mashabiki wameeleza kufurahishwa na namna wanandoa hao wapya walivyoonesha upendo na kuthaminiana katika tukio hilo.
Charlene na Isaya Yunge, ambaye ni mjasiriamali anayejishughulisha na sekta ya teknolojia, walifunga ndoa Novemba 6, 2026, na ndoa yao imeendelea kuvuta hisia za watu ndani na nje ya Kenya.




