Afrika Mashariki

Villa vs Express: Dabi ya kihistoria Uganda

LIGI Kuu Uganda inaendelea leo kwa michezo mitatu ukiwemo wa dabi ya Kampala kati ya SC Villa na Express.

Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Muteesa II uliopo eneo la Wankulukuku jijini Kampala.

SC Villa ndio imetwaa ubingwa mara nyingi zaidi ya Express ikinyakua mara 15, 2004 ukiwa wa mwisho kushinda.

Ingawa Express haijafikia rekodi hiyo lakini ilishinda kwa mara ya mwisho 2020-2021 ikiwa ni mara ya 7.

Miaka iliyopita timu hizo ziliwahi kutamba katika soka la Afrika Mashariki na Kati zikishiki michuano ya Kombe la Challenge.

Katika michezo mingine miwili ya ligi hiyo Gadaffi itakuwa mwenyeji wa NEC wakati Busoga United itakuwa mgeni wa UPDF.

Related Articles

Back to top button