Filamu

Maumivu ya mkono yamsumbua Amitabh Bachchan

MUMBAI: MUIGIZAJI mkongwe wa Bollywood, Amitabh Bachchan, amesema anakabiliwa na maumivu ya mkono yanayomfanya ashindwe kuandika jumbe za kuwashukuru mashabiki wanaomtumia zawadi.

Katika ujumbe aliouchapisha kwenye akaunti yake ya Tumblr wakati wa sikukuu ya Diwali, nyota huyo mwenye umri wa miaka 84 aliwashukuru mashabiki kwa zawadi na salamu nyingi walizomtumia, huku akiomba radhi kwa kuchelewa kuwajibu.

Bachchan alisema alikuwa na nia ya kujibu kila mmoja kupitia barua zilizoandikwa kwa mkono wake mwenyewe, lakini hali ya mkono wake imesababisha kuchelewa kwa zoezi hilo.

Mwezi uliopita, mwigizaji huyo alikuwa ametangaza kusitisha kwa muda machapisho yake ya kawaida mitandaoni baada ya kushauriwa kupumzika na kuendelea na matibabu.

Kwa sasa anaendelea na majukumu ya kuongoza kipindi cha ‘Kaun Banega Crorepati’ pamoja na muendelezo wa maandalizi ya filamu ya ‘Kalki 2898 AD’.

Related Articles

Back to top button