Jamie Foxx, Alyce wamepata mtoto wao wa kwanza

CALIFORNIA: MWIGIZAJI na mwanamuziki, Jamie Foxx na mpenzi wake, Alyce Huckstepp wamepata mtoto wao wa kwanza pamoja.
Alyce, 36 ambaye ni mtaalamu wa ustawi kutoka Australia, huyo ni mtoto wake wa kwanza.
Kwa Jamie huyo ni mtoto wa tatu. Ana mabinti wengine wakubwa Corinne, 32 na Anelise, 18 kutoka kwa wapenzi wake wa zamani, Connie Kline na Kristin Grannis.
Jarida la PEOPLE limeripoti juu ya hilo ikielezwa suala hilo kwa sasa linafanywa siri.
Aidha, hivi karibuni Jamie, 58 alieleza kuwa mwigizaji gwiji, Al Pacino alimfanya ajisikie vizuri zaidi kuhusu kuwa baba tena katika umri huo mkubwa.
Mwezi Mei, mwaka huu iliripotiwa juu ya ujauzito huo, huku vyanzo mbalimbali vikieleza kuwa wakati huo, ujauzito huo ulikuwa tayari una miezi kadhaa.
Jamie na Alyce, walianza kuhusishwa na kimapenzi mwaka 2022 kabla ya kuachana na kurudiana mwaka jana.




