Kwingineko

Real Madrid yamvuta Rafael Nadal

MADRID: KLABU ya Real Madrid imemteua Rafael Nadal kuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya klabu hiyo.

Punde baada ya tangazo hilo, bingwa huyo mara 22 wa mashindano ya Grand Slam, ambaye pia ni shabiki wa muda mrefu wa timu hiyo, akaeleza kukubali wadhifa huo.

Kupitia Mtandao wa X, Nadal alitoa shukran juu ya wadhifa huo, akisindikiza na picha yake ya utotoni akiwa amevaa jezi ya Real.

“Ningependa kumshukuru Rais Florentino Perez na bodi kwa kunipendekeza kuwa sehemu ya Bodi ya Wakurugenzi ya Real Madrid.

“Nimekubali pendekezo hili kwa msisimko mkubwa, nikiwa na hamu ya kujifunza na kutoa mchango wangu wote kadri niwezavyo,” aliandika Nadal.

 

Hiyo, imekuja baada ya Mei, mwaka huu, Nadal, ambaye ni mwanachama wa heshima wa Real, kukanusha taarifa zilizomhusisha na uwezekano wa kugombea urais wa klabu hiyo.

Nayo, Real ilitoa pongezi kwa Nadal, 40, aliyeisaidia Uhispania kutwaa mataji matano ya Davis Cup kabla ya kustaafu kucheza tenisi mwaka 2024.

Lakini pia ilieleza namna gani inaamini kupitia mafanikio na nidhamu yake ndani na nje ya uwanja na kujitolea kwake kutaboresha na kukuza memgi ndani ya Madrid na michezo kiujumla kila kona.

Related Articles

Back to top button