BundesligaKwingineko
Sancho arejea Dortmund kwa mkopo

WINGA wa Manchester United na England Jadon Sancho amerejea kwa mkopo katika klabu yake ya zamani ya Borussia Dortmund kwa kipindi chote kilichobaki cha msimu wa 2023-24.
Sancho, 23, alihamia Old Trafford kutoka Dortmund Julai 2021 kwa dau la pauni mil 73.
“Siwezi kuongoja kuwaona wachezaji wenzangu tena, kwenda uwanjani, kucheza kwa tabasamu usoni mwangu, kutoa pasi za mabao, kufunga mabao na kusaidia timu kufuzu Ligi ya Mabingwa,” amesema Sancho.
Ripoti zimesema mkataba wa mkopo wa Sancho hauna chaguo la kumnunua.
Winga huyo hajacheza United tangu Agosti 26, 2023 baada ya kutofautiana na Kocha Erik ten Hag na amekuwa akifanya mazoezi nje ya kikosi cha kwanza tangu Septemba 2023.