Masumbwi

Salmin: Siri ya ushindi ni kwenda nje

DAR ES SALAAM: BONDIA Mtanzania, Salmin Kassim, amesema siri ya ushindi wake wa KO dhidi ya Jayr Raquinel kutoka Ufilipino Philippines katika pambano la Expensive Fight ni uzoefu alioupata katika mapambano ya nje ya nchi.

Kassim alimpiga Raquinel kwa KO katika raundi ya saba ya pambano hilo lililofanyika Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo, akirejea ulingoni nchini Tanzania kwa ushindi mkubwa.

Akizungumza baada ya pambano hilo, Kassim amesema kushiriki mapambano nje ya nchi kumemsaidia kukutana na mabondia wenye viwango tofauti na kujifunza mbinu mpya zilizomsaidia kuongeza kiwango chake.

“Siri ni kwenda nje ya nchi. Nimeenda kule nikafundwa vitu vingi, nimeenda kushiriki mchezo wa IBO ambao ni mkubwa duniani na nimekutana na mabondia wagumu pia kule nje. Leo mmeona nilichojifunza nje na nilivyoweza kukitumia,” amesema Kassim.

Amesema amefurahishwa kurejea kucheza nchini na kupata ushindi huo, huku akiwashukuru Watanzania na Mafia Promosheni kwa sapoti waliompa kabla na wakati wa pambano hilo.

Related Articles

Back to top button