Masumbwi

Chola atishia kumdondosha Shauri

DAR ES SALAAM: BONDIA Gabriel Chola maarufu kama Mmasai, ametamba kumdondosha mkongwe Ramadhani Shauri wa Mabibo katika pambano la Boxing Day litakalofanyika Desemba 26, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Chola amesema Shauri anakwenda kukutana na bondia mwenye ndoto kubwa ya mafanikio, hivyo anatarajia kutumia pambano hilo kuonesha uwezo wake na kuthibitisha kuwa ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika mchezo huo.

Akizungumza wakati akiendelea na maandalizi yake, Chola amesema anamuheshimu mpinzani wake, lakini haogopi uzoefu wake, akisisitiza kuwa amejipanga kuhakikisha anaibuka na ushindi siku hiyo.

“Mashabiki naomba mjitokeze kwa wingi, nawaahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha natimiza lengo langu la kumshinda Shauri,”amesema.

Takwimu za mtandao wa ngumi za boxrec zinaonesha Chola ameshacheza mapambano 19 na kati ya hayo, ameshinda 10, amepoteza nane na kupata sare moja.

Anatarajia kukutana na Shauri ambaye amecheza mapambano 47 na kati ya hayo, ameshinda 28, amepoteza 18 na kupata sare moja.

Related Articles

Back to top button