Kwingineko

Barcelona yatoa onyo Champions League

ROME, Italia: MABINGWA watetezi wa ligi ya Mabingwa wa Ulaya kwa Wanawake Barcelona, wameendelea na mwanzo mzuri wa mashindano hayo baada ya kuifunga Roma mabao 6-0 katika mchezo wa hatua ya ligi uliochezwa nchini Italia.

Caroline Graham Hansen aliiweka Barcelona mbele ndani ya dakika 20, kabla ya Shukurat Oladipo kujifunga na kufanya Barcelona kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0. Claudia Pina aliongeza bao la tatu mapema kipindi cha pili.

Graham Hansen alifunga bao lake la pili katika mchezo huo na kufikisha mabao matatu katika mashindano hayo, huku Pina akifunga tena kabla ya Ewa Pajor kukamilisha ushindi wa Barcelona kwa bao la sita mwishoni mwa mchezo.

Ushindi huo umeifanya Barcelona kufikisha pointi sita katika michezo miwili ya hatua ya ligi, ikiwa imefunga mabao 11.

Timu hiyo imeanza mashindano hayo bila kuonekana kutetereka licha ya kuondokewa na nyota wake Alexia Putellas aliyejiunga na London City Lionesses msimu huu.

Related Articles

Back to top button